IQNA

Utawala wa Israel umeua shahidi watoto 77 Wapalestina mwaka huu wa 2021

16:48 - November 21, 2021
Habari ID: 3474585
TEHRAN (IQNA)- Taasisi moja ya Haki za Binadamu imeripoti kuwa utawala ghasibu wa Israel umewauwa watoto wa Kipalestina 77 tangu kuanza mwaka huu wa 2021 hadi sasa.

Taasisi hiyo imesema kuwa, ukaliaji mabavu wa Israel umesababisha kuuliwa watoto wa Kipalestina 77 mwaka huu huku wengine kati ya 500 na 700 wakihukumiwa kijeshi kila mwaka. 

Hayo yameelezwa na Taasisi ya Kimataifa ya Kutetea Watoto tawi la Palestina kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Watoto ambayo huadhimishwa tarehe 20 Novemba kila mwaka. 

Taasisi ya The Defense for Children International imeongeza kuwa, imetayarisha matukio ya kuuliwa shahidi watoto wa Kipalestina 77 na risasi za wanajeshi wa Israel tangu kuanza mwaka huu hadi sasa; 61 miongoni mwao wakitoka Ukanda wa Ghaza na 16 katika Ukingo wa Magharibi ikiwemo Quds mashariki.  

Wanajeshi wa utawala haramu wa Kizayuni umewauwa watoto wa Kipalestina wasiopungua 2,200 tangu mwaka 2000 hadi sasa. Taasisi ya The Defense for Children International Tawi la Palestina imeongeza kuwa, mtoto wa Kipalestina anachukuliwa kama mlengwa mkuu wa viotendo vya kila siku vya ukaliaji mabavu kupitia mauaji, kamatakamata ya kiholela, kushambuliwa nyumba za raia wa Palestina na vituo vya elimu licha ya kuwa miongoni mwa maeneo yanayolindwa na sheria na kanuni za kimataifa. 

4014852

Kishikizo: watoto palestina israel
captcha