IQNA

Wanafunzi Waislamu Nigeria wapigania haki ya kuvaa Hijabu

13:31 - November 23, 2021
Habari ID: 3474591
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa Kiislamu katika jimbo la Oyo nchini Nigeria wameapa kupigania haki za wasichana Waislamu kuvaa Hijabu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu katika jimbo hilo Alhaji Kunle Sanni amesema wanapanga kufikisha kesi mahakamani kutaka shule za umma zishurutishwe kuwaruhusu wasichana wavae Hijabu.

Sanni ameyasema hayo Jumapili mjini Ibadan katika kikao cha Jumuiya ya Waislamu wa Jimbo la Oyo kimefanyika chini ya kauli mbiu ya “Umoja wa Waislamu Jimboni Oyo: Chaguo Lisiloepukika”

Sanni amesema hawatakubali tena kisingizio cha kuwazuia wanafunzi Waislamu kuvaa Hijabu katika shule za serikali kwa sababu eti shule hizo ni za Kikristo.

Amebaini kuwa wameamua kufika mahakamani ili tatizo hilo litatuliwa kisheria kwani katiba ya Nigeria inasema, ‘Muislamu ana uhuru wa dini na pia uhuru wa kudhihirisha dini yake na kwa msingi huo Hijabu ni sehemu ya dhihirisho la Uislamu’. Alhaj Sani amesema hadi sasa Waislamu hawajapoteza kesi ya kuvaa Hijabu kwa sababu katiba iko wazi kuhusu suala hilo.

4015320

captcha