IQNA

Maelfu waandamana Jordan kupinga mapatano mapya na utawala wa Israel

11:59 - November 27, 2021
Habari ID: 3474606
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya wananchi wa Jordan wameandamana wakilalamikia mpango wa serikali ya nchi hiyo kutiai saini mapatano mapya na utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamelaani pia  hatua ya nchi kadhaa za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.

Aidha waandamanaji hao wamepinga vikali makubaliano ya nchi yao na utawala vamizi wa Israel ya kubadilishana nishati ya umeme na maji.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, safari ya Benny Gantz Waziri wa Vita wa utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel huko Morocco nayo imekabiliwa na upinzani mkali pamoja na maandamano ya wananchi ambao wametangaza wazi kupinga hatua ya serikali ya rabat ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Itakumbukwa kuwa, Septemba mwaka jana (2020), Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Imarati na Bahrain walisaini mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House mjini Washington.

Baada ya hapo Sudan na Morocco nazo zikafuata mkumbo huo huo na kutangaza  kuanzisha uhusiano na utawala huo haramu, uamuzi ambao umeendelea kulalamikiwa na kulaaniwa na wapenda haki kote ulimwenguni. Mbali na nchi hizo nne, nchi zingine za Kiarabu ambazo zina uhusiano rasmi 

Sudan, Morocco na Bahrain zimeendelea kushuhudia maandamano kila leo ya kulaani na kupinga hatua ya nchi zao ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa  Israel, wakisema kuwa, hatua hiyo ni khiyana na usaliti mkubwa kwa wananchi wa Palestina wanaofanyiwa unyama wa kila aina na utawala huo kila uchao.

/3476665

captcha