IQNA

Wazayuni wapachika alama ya Kiyahudi msikitini

12:33 - November 27, 2021
Habari ID: 3474608
TEHRAN (IQNA)- Walowezi wa Kizayuni Alhamisi wamepachika alama kubwa ya Kiyahudi ijulikanayo kama Menorah katika paa la msikiti wa kihistoria katika kijiji cha An-Nabi Samwil,kaskazini magharibi mwa mji wa Quds (Jerusalem).

Wanakijiji wanasema Wazayuni hao wenye misimamo ya kufurutu ada waliwa wameandamana na maafisa wa utawala haramu wa Israel waliezeka alama kubwa ya menorah katika msikiti wa kijiji hicho kwa ajili ya sherehe ya Kiyahudi ya Hanukkah.

Afisa mwandamizi wa Wizara ya Wakfu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Hussam Abu al Rub amelaani vikali kitendo hicho na kusema kinakiuka na kuvunjia heshima msikiti. Aidha amesema kwa ujumla wanalaani vitendo vya utawala wa Israel kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu kote katika ardhi za Palestina zinazokoloniwa na utawala huo.

Al Rub amesema lengo la utawala wa Kizayuni katika hatua hizo za kichokozi ni kujaribu kufuta utambulisho wa Kiislamu Palestina.

Kijiji cha An-Nabi Samwil kina wakazi takribani 300 na nyumba kadhaa na wakaazi wa kijiji hicho wamezungukwa na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ambao sasa wameanza kujipenyejza ndani ya kijiji hicho.

Hivi sasa kuna walowezi wa Kizayuni wapatao laki saba wanaoishi katika vitongoji vilivyojengwa kinyume cha sheria katika Ukingo wa Magharibi na Quds Mashariki.

Mwaka 2016 na baada ya miaka kadhaa ya walimwengu kusubiri jibu la jamii ya kimataifa dhidi ya ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zilizoporwa za Palestina, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio nambari 2334 linaloitaka Israel isitishe mara moja ujenzi huo katika ardhi zilizoghusubiwa za Palestina.

3476660

captcha