IQNA

Sheikh Zakzaky awakumbuka mashahidi wa mji wa Zaria, Nigeria + Video

18:33 - December 05, 2021
Habari ID: 3474642
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky amezungumza kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa sita wa kumbukumbu ya mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa na jeshi la nchi hiyo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna, dhidi ya wanachama wa harakati hiyo.

Sheikh Zakzaky ametuma risala za rambirambi na kuwazinyooshea mkono wa pole familia za mashahahidi waliouawa katika tukio hilo la kutisha, lililolaaniwa ndani na nje ya Nigeria miaka sita iliyopita.

Kadhalika mwanaharakati huyo wa Kiislamu ambaye ni mtetezi wa wanyonge amekutana na familia familia za wahanga wa mauaji hayo na kuzitaka kuwa na subira na kukubali kadari ya Allah, amezitaka kuwakumbuka daima wapendwa wao waliouawa shahidi.

Katika shambulio hilo la Disemba 12, 2015, inakadiriwa wanachama zaidi ya 1,000 wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria, aghalabu wakiwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia waliuawa kwa kufyatuliwa risasi na jeshi la Nigeria. Miongoni mwa waliouawa walikuwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Katika siku iliyofuata, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria.

Hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi.

4018615

captcha