IQNA

Serikali ya Nigeria yatakiwa izuie kusumbuliwa wasichana wanaovaa Hijabu shuleni

15:57 - December 06, 2021
Habari ID: 3474646
TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Nigeria wamemtaka wazili wa elimu nchini humo Adamu Adamu aingilie kati kuzuia kusumbuliwa wasicana Waislamu wanaochagua kuvaa Hijabu shuleni.

Taasisi ya Kutetea Haki za Binadamu ya Ta'awuni linasema wasichana Waislamu wanaosoma katika  baadhi ya shule na taasisi za kiserikali kusini mwa Nigeria wanasumbuliwa kutokana na uamuzi wao wa kuvaa Hijabu jambo ambalo huenda likaibua ghasia.

Taasisi hiyo  hiyo kupitia mkurugenzi mkuu wake Sulaymon Tadese imetoa wito kwa waziri wa elimu ashughulikie suala hilo kabla ya ghasia kuibuka.

Tadese amesema kuvaa  Hijabu ni amri ya  Mwenyezi Mungu katika sura ya 33 ya Qur'ani Tukufu aya ya 39 isemayo: " *Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Amesema uvaaji wa Hijabu ni kwa mujibu wa kipengee 38 cha Katiba ya Nigeria ya mwaka 1999 iliyofanyikwa marekebisho mwaka 2011 kuhusu uhuru wa kidini, kifikra na maoni. Aidha amesema kuvaa Hijabu ni kwa mujibu wa sheria za Kiislamu za mtu binafsi zinaziruhusiwa Nigeria.

Hivi karibuni pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu katika la Oyo kusini mwa Nigeria Alhaji Kunle Sanni alisema wanapanga kufikisha kesi mahakamani kutaka shule za umma zishurutishwe kuwaruhusu wasichana wavae Hijabu.

Sanni amesema hawatakubali tena kisingizio cha kuwazuia wanafunzi Waislamu kuvaa Hijabu katika shule za serikali kwa sababu eti shule hizo ni za Kikristo.

3476817

Kishikizo: hijabu nigeria
captcha