IQNA

Msahafu ulioandikwa kwa mkono katika maktaba ya kale zaidi ya kitaifa duniani + Video

14:46 - January 09, 2022
Habari ID: 3474782
TEHRAN (IQNA) – Maktaba ya Kitaifa ya Ufaransa ina mjumuiko mkubwa wa maandishi ya Kiislamu ambayo yamekuswanywa katika muda wa karne kadhaa.

Katika maandishi hayo ya Kiislamu yaliyoandikwa kwa mkono,  kuna Misahafu na kurasa za aya za Qur'ani.

Maktaba ya Kitafa ya Ufaransa ambayo ni mashuhuri kama  Maktaba ya  François-Mitterrand iko karibu na Jumba la Makumbusho la Louvre  mjini Paris na hakuna malipo kwa wanaoingia hapo.

Katika kitengo cha maandishi ya kale ambayo klianzishwa mwaka 1821 kuna takribani jildi 250,000 za zama mbali mbali na kwa lugha mbali mbali. Kwa mfano katika kitengo hicho kuna jildi elfu 10 za misahafu au nakala za kale za Qur'ani tukufu zenye thamani kubwa ya kiturathi.

Codex Paris-Metropolitan

Maktaba ya Kitaifa ya Ufaransa pia inakitengo maalumu cha ulimwengu wa Mashariki ambapo kuna vitabu kwa lugha za Kifarsi, Kiarbau, Kituruki, Kiibrania, Kihindi na Kijapani. Kwa mfani kuna karibu jildi 5000 za vitabu vya Kifarsi kuhusu fasihi, historia na utamaduni wa Iran.

Aidha kuna nakala nyingi zenye thamani za vitabu vingi vya Kiislamu ambavyo vimekusanywa kwa muda karne kadhaa. Katika kitengo hicho cha vitabu vya Kiislamu vipatavyo 1200 kuna eneo kubwa lenye misahafu ya kale iliyoandikwa kwa mkono. Kwa mfano kuna Msahafu wa kale ambao unanasibishwa na msikiti mmoja katika mji Fustat nchini Misri ambapo kurasa 70 za mshahafu huo zimewekwa katika maktaba hiyo.

4026527

Kishikizo: paris misahafu
captcha