IQNA

Mchujo wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran waendelea

23:36 - January 15, 2022
Habari ID: 3474811
TEHRAN (IQNA)-Majaji wanaendelea kusikliza klipu zilizotumwa na washiriki wa awamu ya mchujo ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, majaji walisikiliza kwa makini klipu zilizorekodiwa na washiriki katika kategoria mbali mbali na kuwapa alama ili hatimaye ibainike watakaosonga mbele.

Washiriki ambao walituma klipu zao wameweza kushuhudia zoezi hilo la majaji kwa njia ya intaneti kupitia lini walioyotumiwa.

Washiriki ambayo wanajumuisha waliohifadhi Qur'ani na wasomaji kutoka nchi 69 wanashiriki katika mashindano ya kimataifa ya mwaka huu.

Duru ya mchujo ya mashindano inafanyika kwa njia ya intaneti ambapo watakaofaulu watashiriki fainali katika mashindano yatakayofanyika nchini Iran baadaye mwezi Machi mwaka huu na hilo litategemea hali ya janga la COVID-19 duniani.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashidano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran kila mwaka.

 

 

4028511

captcha