IQNA

Mchezaji wa tennis Mkuwaiti apongezwa kukataa kucheza na Muisraeli

17:08 - January 22, 2022
Habari ID: 3474836
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji maarufu wa tennis kutoka Kuwait amepongezwa kwa hatua yake ya kujiondoa katika shindano moja la kimataifa baada ya kubainika kuwa alitakuwa ashindane na raia wa utawala haramu wa Israel.

Muhammad Al Awadi alijiondoa katika Mashindano ya J4 Dubai ambayo yamefanyika katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuanzia Januari 17 hadi 22.

Wanaharakati katika mitandao ya kijamii wamempongeza Mkuwaiti huyo kwa kukataa kuwa sehemu ya sera za kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unazikoloni na kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Yusuf al Sanad, mwanachama wa Jumuiya ya Wasomi wa Ghuba ya Uajemi amesema kijana huyo shujaa wa Kuwait ametangaza kujitoa katika shindano hilo kama njia ya kubainisha kufungamana kwake na Wapalestina na kupinga ugaidi wa Israel.

Naye mbunge mwandamizi wa Kuwait Osama al Shaheen ametuma ujumbe katika Twitter na kuandika" "Salamu na sukrani kwa shujaa wa Kuwait Muhammad al Awadi kutokana na hatua yake ya kupinga uhusiano wa kawaida wa kimichezo na Wazayuni."

Nayo Jumuiya ya Vijana wa Al Quds imeandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ni usaliti na kwamba hatua ya mchezaji huyo wa Kuwait inapaswa kupongezwa na wote.

Hivi karibuni pia katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo y 2020 iliychezwa mwaka jana, wanamichezo wa Sudan na Algeria walikataa kushindana na wanamichezo wanaowakilisha utawala haramu wa Israel.

Aidha wanamichezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu hawakubali hata kidogo kushindana na wanamichezo wa utawala haramu wa Israel kutokana na kuwa Iran haiutambui rasmi utawala huo unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.

4030239

captcha