IQNA

Misikiti ya Oman yaruhusiwa kuwa na asilimia 50 ya waumini

12:36 - January 23, 2022
Habari ID: 3474841
TEHRAN (IQNA)-Oman imetangaza hatua ambazo zinaanza kutekelezwa Januari 23 kufuatia ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19.

Kati ya hatua hizo ni kuwa, misikiti sas aitaruhusiwa tu kuwa na asilimia 50 ya waumini wanaoweza kuswali ndani ya ukumbi asili. Kwa mfano iwapo msikiti una uwezo wa kuwapokea waumini 500 kuanzia sasa watakaruhusiwa kuswali dani ya jengo kuu la msikitni ni 250.

Aidha idara zote za serikali pia nazo zinatakiwa kutekeleza sheria hiyo ya kuruhusu asilimia 50 ya wafanyakazi huku makongamano yote yakipigwa marufuku.  Aidha sala za Ijumaa zimesimamiwshwa kwa muda na ni sala za jamaa za kila siku zitakazoruhusiwa misikitini kwa kuzingatia kanuni za kuzuia kuenea COVID-19. Halikadhalika wote wanaofika katika maduka makubwa na maeneo mengine ya kibiashara wanatakiwa kuwa na chanjo ya COVID-19 na ni sharti kuvaa barakoa, kuepusha msongamano na watu kutokaribiana.

Mapema mwezi huu Oman pia ilitangaza kufunga shule kwa mwezi moja na watoto watasoma kwa njia ya intaneti ili kuzuia maambukizi. Hadi kufikia sasa watu 4,125 wamepoteza maisha kutokana na COVID-19 nchini Oman.

3477480

Kishikizo: oman msikiti covid 19
captcha