IQNA

Msomi: Ni dhambi kuingia msikitini ukijua una COVID-19

13:59 - January 25, 2022
Habari ID: 3474850
TEHRAN (IQNA)- Kuingia msikitini ukiwa unafahamu kuwa unaugua COVID-19 ni dhambi , amesema msomi wa Kiislamu huku akiwataka waumini wazingatia kanuni za kuzuia kuenea COVID-19.

Akizungumza na TV ya Qatar, Sheikh Khalid Abu Moza, mhubiri na mhadhiri wa Kiislamu, anasema waumini wanapaswa kuchukua hatua za kuzuia maambukizi na wakiambukizwa wasali nyumbani.

“Walioambukizwa wanapaswa kuswali nyumbani kwa ajili ya usalama wa wengine na kila anayeingia msikitini akijua kuwa ameambukizwa basi ni mtenda dhambi,” amesema.

Aidha amesisitiza kuhusu kuzingatia kanuni zilizowekwa misikitini ili kuzuia maambukizi ya COVID-19 na amsema waumini walioko Qatar wanapaswa kuonyesha hali yao ya kiafya kupitia aplikesheni ya Ehteraz na wafuata maagizo ya wasimamizi ya misikiti.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar imetangaza kanuni za kufuatwa na waumini wanaofika misikitini kwa maslahi ya afya ya umma. Kati ya masharti hayo ni kuonyesha kibali cha kutougua COVID-19 na pia ni sharti kila moja abebe mkeka binafsi wa kusali sambamba na kuvaa barakoa na kutokaribiana.

3477528

Kishikizo: qatar covid 19 msikiti
captcha