IQNA

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran

Mbinu aliyotumia Imam Khomeini (MA) ilikuwa ni kuwategemea wananchi

17:07 - February 02, 2022
Habari ID: 3474883
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema Mapinduzi ya Kiisalmu ya Iran ni tafauti kabisa na mapinduzi mengine dunaini na kuongeza kuwa: "Mbinu aliyotumia Imam Khomeini (MA) ilikuwa ni kuwategemea wananchi."

Hujjatul Islam wal Muslimin Gholam-Hossein Mohseni-Ejei Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran alipofika katika Haram ya Imam Khomeini MA, akiwa ameandamana na maafisa wa ngazi za juu wa Idara ya Mahakama kwa mnasaba wa kuwadia mwaka  wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Wakiwa hapo wamesoma Surat al Fatiha na kutoa heshima zao kwa Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  sambamba na kujadidisha utiifu wao kwa malengo yake matakatifu. 

Hujjatul Islam wal Muslimin Mohseni-Ejei amesema Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa nuru ambayo ilienea kutokana na ikhlasi ya Imam Khomeini MA na hivyo kuleta uhai mpya katika Uislamu. 

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulitokana na wananchi kumtii Imam Khomeini MA na kuongeza kuwa, Imam Khomeini MA naye aliwaamini wananchi na kutokana na kauli yake ya ukweli na kumtegemea Mwenyezi Mungu, mapinduzi ya kipekee ya Kiislamu yaliweza kupata ushindi.

Mohseni-Ejei amesisitiza kuwa, Uislamu na wananchi ni sifa mbili za Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa, Imam aliwaamini wananchi na kushauriana nao katika mambo mengi.

4033353

captcha