IQNA

Mchezaji wa kandanda kimataifa Ghana ajenga msikiti

15:57 - February 22, 2022
Habari ID: 3474961
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji kandanda wa kimataifa wa Ghana Abdul Majeed Waris anajenga msikiti wa orofa mbili kwa ajili ya jamii ya Waislamu katika mji aliozaliwa.

Waris anayechezea timu ya Racing Strasbourg katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) anafadhili kikamilifu mradi wa msikiti, ambao uko Lamashegu huko Tamale.

Ukurasa wa Twitter wa taasisi ya misaada ya mchezaji huyo imesambaza picha za msikiti na kufichua kuwa kazi ya mradi ilikuwa ikiendelea kwa mafanikio.

Ujumbe wa Twitter wa taasisi hiyo umeandamana na piche yenye maelezo yasemayo, "Hali ya sasa ya Msikiti wa jengo la ghorofa mbili unaojengwa katika jumuiya ya Lamashegu huko Tamale, Mkoa wa Kaskazini wa Ghana. Mradi huo unafadhiliwa kikamilifu na mwanzilishi wetu ambaye ni mtu kawaida.”

Wakati huo huo, Waris pia ameandika ujumbe na kusema amefurahishwa e na mradi unaoendelea katika mji wake.

"Nimefurahi hatimaye kuona mradi huu mzuri ukichukua sura," aliandika, akiandamananisha picha ya msikiti huo.

Waris alizaliwa Lamashegu huko Tamale, mji mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, na kwa sasa anachezea Racing Strasbourg ya Ligue 1 ya Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ameshiriki mara 16 katika mechi za Ligue 1 msimu huu na amefunga mabao mawili hadi sasa.

Waris anajulikana kwa kurudisha nyuma kwa jamii na, mnamo 2021, alilipa makandarasi kukarabati barabara ya Lamashegu ambayo ilikuwa katika hali ya kusikitisha.

/3477915/

captcha