IQNA

Mtaalamu wa Morocco: Nchi zingine ziige mfano wa mashidano ya Qur'ani ya Iran

16:04 - March 05, 2022
Habari ID: 3475007
TEHRAN (IQNA)- Mtaalamu wa masuala ya Qur'ani kutoka Morocco amepongeza utaratibu bora katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran mwaka huu.

Katika mahojiano na IQNA, Mohammad Ali Attafi ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa mashindano ya Qur'ani kwa muda mrefu na kuongeza kuwa hata mashindano yaliyofanyika kwa njia ya intaneti mwaka huu yamefana.

Fainali ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran iliyoanza Jumatatu iliyopita inatazamiwa kumalizika leo Jumamosi usiku mjini Tehran.

Attafi ambayo ni mtaalamu wa fani za Waqf na Ibtida katika usomaji Qur'ani amesema huu ni mwaka wa nne ambao yeye ni jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran.

Mtaalamu huyo wa Morocco amesema mashindano ya mwaka huu yamekuwa fursa nzuri kwa vijana kuimarisha vipji vyao wa kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Mbali na Wairani mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran mwaka huu pia yalikuwa na majaji Wapakistani, Wairaqi na kutoka Jordan.

Jumla ya makari 62 na wahifadhi Qur'ani kutoka nchi 29 wanashindana katika hatua hii ya mashindano hayo, ambayo inafanyika karibu.

Sambamba na hilo, shindano la 5 la kimataifa la Qur'ani kwa wenye ulemavu wa macho, shindano la 7 la kimataifa la Qur'ani kwa wanafunzi wa shule, na mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake pia yanafanyika.

Kwingineko katika matamshi yake Athamina alibainisha kuwa amesafiri nchini Iran mara 13 kuhudumu kama mjumbe wa jopo la majaji katika mashindano tofauti ya kimataifa ya Qur'ani.

Amebainisha kuwa hivi sasa anaongoza jopo la wanazuoni nchini Jordan lililopewa jukumu la kusimamia uchapishaji wa Qur’ani nchini humo.

Pia amesema ana watoto watatu wa kiume na wa kike wawili ambao wote ni wahifadhi wa Quran.

4040320

 

captcha