IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran kufanyika Mwezi wa Ramadhani

21:07 - March 13, 2022
Habari ID: 3475036
TEHRAN (IQNA)- Duru ya 29 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran imepenga kufanyika katika Ukumbi wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini (RA).

Kwa mujibu wa Ali Reza Moaf Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur’ani Tukufu na Ertat amesema maonyesho hao yatafanyika kwa muda wa siku 12 katika nusu ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema maonyesho hayo yamepangwa kuanza 15 hadi 27 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani (Apirli 17-29) na kwamba kila atakayeingia katika ukumbi wa maonyesho atatakiwa kuzingatia kanuni zote za kiafya ambazo zitatangazwa.

Moaf amesema awali walipanga maonyesho yafanyike kwa muda wa siku 25 lakini Idara ya Kitaifa ya Kupambana na Corona Iran imetoa idhini ya maonyesho kufanyika kwa muda wa siku 12 huku kukiwa idadi ndogo ya watakaokuwa na vibanda katika maonyesho ya mwaka huu.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza baada ya miaka miwili kwa maonyesho ya Qur’ani Tukufu kufanyika katika ukumbi tokea janga la corona lianze. Mwaka 2020 na 2021 maonyesho hayo yalifanyika kwa njia ya intaneti kutokana na janga la coron. Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yamekuwa yakiandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu kila mwaka na yanalenga kustawisha ufahamu na harakati za Qur’ani nchini Iran.

4042286

captcha