IQNA

Sala ya Idul Fitr katika eneo la Bayn al-Haramayn baada ya kusitishwa miaka miwili

21:22 - May 04, 2022
Habari ID: 3475203
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya waumini wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr katika eneo lililo baina ya Haram Mbili Takatifu za Imam Hussein AS na Hadhrat Abbas AS linalojulikana kama Bayn al-Haramayn katika mjini Karbala, Iraq.

Hii ni mara ya kwanza kwa Sala ya Idi kusaliwa hapo  baada ya kusitishwa kwa miaka miwili kutokana na maambukizi ya corona ambayo sasa yamepungua sana nchini Iraq.

Sala ya Idul Fitr imesalishwa na Sheikh Murtadha Qazwini ambaye ametoa wito kwa waumini kumshukuru Allah SWT kwa kujaalia Haram Takatifu za Ahul Bayt wa Mtume Muhammad SAW katika miji ya Iraq.

Aidha ameipongeza serikali ya Iraq kwa kuimarisha usalama  nchini humo. Sala ya Idi imesaliwa mara kadhaa katika eneo hilo jana kutokana na idadi kubwa ya waumini  walioshiriki.

Maelfu ya Waislamu wa Iraq jana walishiriki katika Sala ya Idul Fitr baada ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Baadhi ya mataifa ya Kiislamu kama Saudi Arabia, Uturuki, Misri, Qatar, Kuwait na Palestina yaliadhimisha sikukuu ya Idul Fitr jana huku mataifa mengine ya Kiislamu kama Iran, Tanzania, Pakistan na Iraq yakisherehekea sikukuu hiyo Jumanne ya jana.

 

 

4054762

captcha