IQNA

Benki za Kiislamu

Benki ya Kiislamu ya Pakistan zitazipiku za kawaida ifikapo 2026

18:27 - May 25, 2022
Habari ID: 3475293
TEHRAN (IQNA) - Sekta ya benki ya Kiislamu ya Pakistani inakadiriwa kuwa inastawi haraka na hivyo itazipita kwa kiasi kikubwa benki za kawaida ifikapo 2026.

Haya ni kwa mujibu wa Huduma ya Wawekezaji ya Moody's.

"Ukuaji mkubwa katika muongo uliopita hauonyeshi dalili za kupungua. Sekta ya benki ya Kiislamu nchini Pakistani imekua kwa asilimia 24 kwa mwaka kwa wastani katika muongo mmoja uliopita na ilipanuka kwa asilimia 30.6 mwaka 2021 pekee,” Moody’s ilisema katika ripoti yake ya hivi punde Jumanne.

"Tunatarajia ukuaji wa benki za Kiislamu utaendelea kushinda huduma za benki za kawaida, na kuweza kuwa na asilimia karibu 30 ya fedha zilizwekwa benki ifikapo mwisho wa 2026," ilisema ripoti hiyo ikihusisha ukuaji huu na mchanganyiko wa idadi kubwa ya watu wa Pakistan ambao karibu wote ni Waislamu."

Ripoti hiyo imebaini kuwa  mali za benki za Kiislamu zilistawi kwa wastani wa asilimia 24 kwa mwaka katika muongo mmoja uliopita hadi dola billioni 31.2, ikichukua takriban asilimia 19 ya jumla ya mali zote za benki, kutoka asilimia 8 mwaka 2011. Inatabiriwa kuwa ukuaji wa kila mwaka wa zaidi ya asilimia 25 katika kipindi cha miaka mitano ijayo, utapelekea kuongeza sehemu ya soko ya sekta ya benki za Kiislamu  hadi karibu asilimia 30

Pamoja na hayo ushirikishwaji wa wananchi katika mfumo wa kifedha nchini Pakistan bado ni mdogo, licha ya maendeleo ya hivi karibuni; kulingana na Benki ya Taifa ya Pakistani (SBP) takriban asilimia 62 ya idadi ya watu wazima nchini humo wana akaunti na taasisi rasmi ya kifedha, katika hali ambayo kiwango hicho ni asilimia 95 katika nchi za kipato cha juu.

Sekta ya benki ya Kiislamu nchini Pakistani inajumuisha taasisi 22 za benki za Kiislamu, zikijumuisha benki tano za Kiislamu zenye mamlaka kamili na benki 17 za kawaida ambazo zina matawi ya benki ya Kiislamu. Jumla ya matawi 3,956 yalikuwa yakifanya kazi kufikia Desemba 2021, na madirisha 1,442 ya ziada ya benki za Kiislamu (kaunta za Kiislamu katika matawi ya kawaida). Mwaka 2021, matawi 500 yaliongezwa. Moody's inataraji kuwa , kwa uchache idadi hiyo ya matawi mapya itaongezeka kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kuongezeka kwa matumizi ya njia za dijitali na kielektroniki pia kutasaidia ukuaji beki za Kiislamu. Kwa kuzingatia uwezo wa ukuaji wa sekta hii na utendaji dhabiti wa kifedha, "tunatarajia benki nyingi zaidi kutuma maombi ya leseni za benki za Kiislamu na kwa benki za kawaida kubadilisha muundo na kuwa benki za Kiislamu kikamilifu" kama hivi majuzi, Faysal Bank Ltd, benki ya ukubwa wa kati yenye inayoshikilia asilimia 3 ya soko la Pakistan, imeanza mchakato wa kubadilisha muundo kutoka benki ya kawaida hadi ya Kiislamu.

Sio tu katika utendaji thabiti wa kifedha, taasisi za benki za Kiislamu nchini Pakistani pia zina faida zaidi kuliko zile za kawaida na utendaji wao katika mikopo ni bora zaidi.

3479049

captcha