IQNA

Qur'an Inasemaje /11

Ni vipi tutampokonya silaha Shetani?

18:33 - June 24, 2022
1
Habari ID: 3475417
TEHRAN (IQNA)-Tunamjua Mwenyezi Mungu kuwa ni Mwingi wa Rehema na Mwenye kurehemu. Kwa hiyo Mungu hatatuacha peke yetu mbele ya adui yetu mkuu, yaani Shetani.

Majaribu, hila na hadaa ni njia zinazotumiwa na Shetani kuwapotosha wanadamu. Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, uadui wa Shetani na wanadamu ulianza pale mwanadamu alipoumbwa. “ Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi..” (Surah Al-Baqarah, aya ya 208)

Ingawa Shetani hana mamlaka juu ya mwanadamu, anaweza kumpoteza kwa njia kama vile majaribu, udanganyifu, n.k. Lakini je, mwanadamu hana ulinzi kamili mbele ya Shetani?

Qur'ani Tukufu, baada ya kumtambulisha Shetani na njia anazotumia kupenyeza moyo wa mwanadamu, inatoa njia za kukabiliana na tishio la Shetani.

Hatua ya kwanza ili kukabiliana na Shetani na kuitakasa nafsi ya mtu kutokana na uchafu unaosababishwa na vishawishi vya Shetani ni Tawbah (toba). Hatua ya kwanza mbaya iliyochukuliwa na mwanadamu ilirekebishwa na Tawbah: “Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.” (Surah Al-Baqarah, aya ya 37)

Umuhimu wa Tawbah ni kwamba kama mtu atafanikiwa kutubia na akafanya matendo mema baadaye, Mwenyezi Mungu hatamsamehe dhambi yake tu bali pia atageuza maovu yake kuwa mema: dhambi kubadilishwa na wema; Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.” (Surah Al-Furqan, aya ya 70)

Hatua nyingine ni kumkumbuka Mungu kwa moyo wote. Hili ni hitaji la nafsi na huzuia majaribio ya Shetani kumjaribu mwanadamu. “Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru.” (Surah Al-Ahzab, aya ya 41)

Kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani, kuwa na Taqwa (kumcha Mungu), kujiepusha na dhambi, na Tawakkul (kumtegemea Mungu) ni njia nyinginezo za kumshinda Shetani na kuepuka upotofu. " Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi." (Surah An-Nahl, aya ya 99).

Habari zinazohusiana
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
ahmed juma
0
0
hakika ya mola wetu mlezi amemuumba mwana dabu kwa lengo la kumtambua na kufuata muongozo wake uliokuja kwa vigezo tofauti kama Quran hadithi na sunna za prophet mohmmad (SAW).hivyo bas inahitajika subra na uvumilivu juu ya majarbio na mitihani tunayoiptia hakika ya Allah yupo pmja na wenye kusubir na hawatojutia juu ya uvumilivu wao. Allah atupe muongozo tufikie lengo na atufishe tukiwa katka njia ya kalima ya Laailaha illa Allah Muhammad rasulullah.insha Allah
captcha