IQNA

Ibada ya Hija

Maelfu ya Waislamu waendelea kuwasilia Makka kwa ajili ya Hija

19:34 - July 01, 2022
Habari ID: 3475446
TEHRAN (IQNA) - Maelfu ya waumini wa dini tukufu ya Kiislamu kutoka kona zote za dunia wameendelea kuwasili katika mji mtakatifu wa Makka Ijumaa, wakiwa ni miongoni mwa Waislamu milioni moja wanaotarajiwa kushiriki ibada ya Hija mwaka huu wa 2022 ambapo hii ni mara ya kwanza baada ya miaka miwili ya kuzuia mahujaji kutoka nje ya Saudia kutokana na janga la Covid.

Waumini wakiwa wamevalia mavazi meupe ya Ihramu, na baadhi wakiwa na mwavuli wa kujikinga na jua kali, wametukfu au  kuzunguka Kaaba tukufu katika Msikiti Mkuu wa Makka.

" Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu.... haiwezekani kuelezea hisia zangu hivi sasa," Ahmed Sayed Mahmoud, amesema hujaji kutoka Misri. "Kuwa katika Msikiti Mkuu wa Makka na katika ardhi hii ya Misikiti Miwili takatifu kunanifurahisha sana."

Kuna misikiti miwili mitakatifu zaidi katika Uislamu Saudi Arabia, ambayo ni Msikiti Mkuu wa Makka, Al Masjid Al Haram mjini Makka na Al-Masjid an-Nabawi mjini Madina. Mwaka huu Saudia imeruhusu Waislamu kutoka nje ya ufalme huo kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu baada ya miaka miwili.

Ni raia elfu chache tu wa Saudia na wakaazi wa kigeni nchini humo walihudhuria Hija ya kila mwaka katika miaka miwili iliyopita wakati Covid-19 ilisababisha shida katika usafiri duniani

Mwaka huu ni Waislamu  milioni moja tu watakaotekeleza ibada ya Hija, chini ya nusu ya viwango vya kabla ya Covid, na wanaoruhusiwa ni wenye umri wa miaka 18 hadi 65 ambao wamechanjwa kikamilifu na hawana magonjwa sugu. Waumini wataendelea kuingia Saudia kabla ya kuanza ramsi ibada ya Hija siku chache zijazo.

3479527

captcha