IQNA

Vikao vya kubaini uwezo wa waliohifadhi Qur'ani vyafanyika katika Misikiti ya Gaza

18:12 - July 26, 2022
Habari ID: 3475543
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu katika Ukanda wa Gaza imeandaa vikao katika misikiti miwili katika eneo hilo lililozingirwa la Palestina ili kutathmini ujuzi wa Qur’ani Tukufu wa wavulana na wasichana waliohifadhi Qur'ani Tukufu.

Wavulana 12 na wasichana 19 ambao ni wanafunzi wa Taasisi ya Qur'ani Tukufu ya Gaza walihudhuria kikao hicho.

Kikao hicho kilifanyika chini ya anuani ya la "Qiraa ya Qur'ani Tukufu Kikamilifu Katika Kikao Kimoja.

Msikiti wa Khalid ibn Walid uliandaa kikao ajili ya wasichana huku kikao cha wavulana kilifanyika katika Msikiti wa al-Hassayina.

Maafisa kadhaa akiwemo Naibu Waziri wa Wakfu Abdul Hadi al-Agha, mkurugenzi wa idara ya masuala ya Qur'ani Muhammad Salim, mkurugenzi wa idara ya kuhifadhi Qur'ani Zyad Ahmed, na mkurugenzi wa idara ya mafunzo ya Qur'ani Hamid al-Najjar walisimamia utekelezaji wa mpango huo.

Hotuba ya Al-Agha ilipongeza mkusanyiko wa wavulana na wasichana katika nyumba za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kusoma Quran.

Pia alisifu mapokezi mazuri ya matukio ya vikao vya kiroho kama vile programu za Qur'ani katika Ukanda wa Gaza.

Afisa huyo alielezea matumaini ya kufikiwa kwa malengo katika nyanja za Qur'ani.

Shughuli za Qur'ani ni za kawaida sana katika Ukanda wa Gaza na programu za usomaji Qur'ani hufanyika huko kwa mwaka mzima.

 

Inafaa kuashirikia hapa kuwa shughuli za Qur'ani zinaendelea katika Ukanda wa Gaza pamoja na kuwa eneo hilo liko chini ya mzingiro wa kinyama uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kwamba kuzingirwa kwa miaka 15 kwa Ukanda wa Gaza kumesababisha maafa makubwa katika eneo hilo.

Tangu mwaka 2006 utawala wa Kizayuni wa Israel umeliweka eneo la Ukanda wa Gaza chini ya mzingiro wa pande zote. Sababu kuu ya mzingiro wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza ni ushindi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika uchaguzi wa Bunge la Palestina na kushindwa harakati ya Fat'h, na vilevile makubaliano ya kiusalama kati ya Misri na utawala wa Kizayuni. Ijapokuwa serikali iliyotokana na uchaguzi huo wa Bunge la Palestina ilisambaratika kutokana na mizozo ya ndani, na harakati ya Fat'h ikachukua tena madaraka, lakini mzingiro wa utawala wa Israel haujaisha na unaendelea hadi hii leo licha ya kupita miaka 15 sasa. 

Kutokana na mzingiro huo, Gaza imekumbwa na maafa makubwa. Kuzingirwa kwa miaka 15 eneo la Gaza kumesababisha uhaba wa chakula katika eneo hilo kiasi kwamba, Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo la umoja huo (FAO) pia wameeleza wasiwasi wao kuhusu suala hilo. Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Kisiasa na Kiuchumi cha Palestina, mwaka 2021 zaidi ya nusu ya familia za Wapalestina hazikuwa na usalama wa chakula.

3479841

captcha