IQNA

Ibada ya Umrah

Saudia yasema si sharti tena kuwa na chanjo kuingia Msikiti wa Makka, Msikiti wa Mtume

16:10 - August 03, 2022
Habari ID: 3475574
TEHRAN (IQNA) – Waumini ambao hawajachanjwa sasa wanaruhusiwa kuingia katika maeneo mawili matakatifu zaidi ya Uislamu ambayo ni Msikiti Mtakatifu wa Makka (Masjid al-Haram) na Msikiti wa Mtume (Al-Masjid an-Nabawi) mjini Madina.

Haya ni kwa mujibu wa Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia. Waislamu ambao hawajachanjwa wanaruhusiwa kuingia kwenye Masjid al-Haram na Al-Masjid an-Nabawi kwa ajili ya Sala na Hija ndogo ya Umrah kwa sharti kwamba hawajaambukizwa au hawajawasiliana na mgonjwa wa COVID-19, wizara hiyo ilisema

"Watu ambao hawajachanjwa wameruhusiwa kusali katika misikiti miwili mitakatifu na kupata vibali kupitia programu ya Eatmarna kufanya Umrah, mradi hawajaambukizwa au kuwasiliana na mgonjwa wa COVID-19," ilieleza.

Msimu mpya wa Umrah ulianza Jumamosi, kwa mnasaba wa tarehe Mosi Muharram ambayo ni mwanzo wa mwaka mpya wa Kiislamu wa Hijiri.

Mamlaka katika ufalme huo zimejipanga kwa msimu mpya unaotarajiwa kuvutia zaidi ya Waislamu milioni 10, kulingana na maafisa wa Saudia.

3479947

captcha