IQNA

Siku ya Ashura

Nafasi ya wanawake katika mwamako wa Ashura

16:17 - August 10, 2022
Habari ID: 3475602
TEHRAN (IQNA) – Nafasi ya wanawake katika mwamko wa Ashura yote imekuwa chanya. Sio tu kwamba kuna jukumu la wanawake wa kipekee kama Bibi Zaynab (SA) na Umm Salama, lakini pia hakuna ukandamizaji uliotekelezwa na na wanawake na kwani hata wake wa baadhi ya makamanda wa jeshi la Yazid bin Muawiya wamewakemea waume zao.

Mwanazuoni wa chuo kikuu Marziyeh Mohammadzahed katika hotuba kwenye kongamano lililopewa jina la "Wanawake Waliomsaidia Imam Hussein (AS), alifafanua juu ya nafasi ya wanawake katika mwamko wa  Ashura. Nukuu kutoka kwa hotuba yake ni kama ifuatavyo:

Katika harakati ya Imam Hussein (AS) kulikuwa na makundi mawili ya wanawake. Moja ya makundi haya yametajwa katika historia. Walikuwa ni wale walioondoka Madina wakifuatana na Imam Hussein (AS) na kwenda Karbala, kisha Shaam na baadaye wakawasili Madina kwa ushindi. Miongoni mwao alikuwa Bibi Zaynab (SA).

Kundi la pili linajumuisha wale ambao walikuwa na nafasi katika harakati hiyo lakini hawakufuatana na msafara wa Imam Hussein (AS) kwenda Karbala kwa sababu fulani. Kwa mfano Umm Salama ilimbidi abaki Madina au mama na mke wa Hazrat Abbas (AS) walikuwa Basra wakati huo. Pia katika kundi hili wamo wake wa makamanda wa jeshi la Yazd bin Muawiya. Waume zao walihusika na ukatili lakini wao wenyewe walikuwa wakiunga mkono njia ya Imam Hussein (AS).

Mmoja wa wanawake ambao walikuwa na jukumu katika harakati hiyo alikuwa Mariya, ambaye baba yake na mume wake walikuwa wameuawa kishahidi katika Vita vya Jamal. Alikuwa tajiri na nyumba yake huko Basra ikawa kituo cha kuwapokea masahaba wa Imam Hussein (AS).

Wanawake wa mwamako wa kihamasa wa Karbala walimjua vyema Imamu wao na walijitolea yote waliyokuwa nayo kwenye njia yake. Mmoja wao ni mama yake Omar ibn Janada ambaye mume wake aliuawa kishahidi mapema siku ya Ashura. Alimpeleka mwanawe kwenye uwanja wa vita na baada ya kuuawa kishahidi na adui akampeleka mtoto wake kwa mama, alijibu kwa kusema, “Tumeshinda; chukua  kichwa tulichokitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu."

Wanawake wa vuguvugu hilo pia walikuwa na ufahamu mkubwa kuhusu matukio ya wakati huo. Mke wa Zuhayr ibn al-Qayn alikuwa mmoja wao. Zuhayr alikuwa katika jeshi la adui lakini mke wake alimhimiza kujiunga na jeshi la Imam Hussein (AS) na aliuawa kishahidi huko Karbala.

Wanawake wa Karbala pia walikuwa wasimamizi waliofaulu ambao walijua jinsi ya kusimamia hali hiyo kwa kutambua nguvu na udhaifu na kutenda vyema zaidi. Ilikuwa ni kutokana na jinsi Hazrat Zaynab (SA) alivyoisimamia hali hiyo kwamba hakuna hata mmoja wa watoto hao aliyeumizwa au kupotea katika saa hizo za machafuko na siku baada ya Vita vya Karbala kumalizika na Imam Hussein (AS) na masahaba wake wote waliuawa kishahidi.

Katika jamii yenye nguvu ya Kiislamu, wanaume na wanawake wanapaswa kuwa katika eneo la tukio katika masuala yote ya kisiasa, kijamii na kiutamaduni, ikiwa ni pamoja na kuhumiza mema na kukataza maovu.

captcha