IQNA

Tafakari

Uhusiano kati ya elimu na hekima katika maisha ya Waumini

23:50 - August 12, 2022
Habari ID: 3475615
TEHRAN (IQNA) – Ingawa elimu ina hadhi ya juu katika ustawi wa mwanadamu lakini inahitaji kuunganishwa na hekima ili kuibua kielelezo cha maisha ya mwanadamu.

Elimu ni ufahamu kuhusu maelezo yanayoweza kupatikana kwa kusoma, kujifunza na uzoefu. Lakini ili elimu itumike ipasavyo maishani inahitaji kuandamana hekima.

Elimu sio kinyume cha ujahili (ujinga). Kuna Hadithi kutoka kwa Ahl-ul-Bayt (AS) kuhusu baadhi ya watu wenye  elimu ambao ujahili wao umewapeleka kwenye maangamizo. Kwa hiyo ujahili sio kinyume cha elimu. Kwa mtazamo wa Qur’ani Tukufu, kinyume cha ujahili nihekima. Hivyo ili kuwa na manufaa, elimu inapaswa kupita kwa hekima na kuchakatwa.

Kwa mtazamo wa aya za Qur’ani na Hadith, hekima, subira na Taqwa (kumcha Mungu) vinaweza kusaidia kufanya elimu kuwa nuru inayomulika mtu maishani. Kwa hiyo ujinga au ujahilia si sawa na kutokuwepo ufahamu. Mara nyingi kuna elimu na maarifa lakini pamoja na hayo mtu huwa jahili kwa sababu ya kushindwa kutumia hekima katika anachofanya. Hekima inahitaji elimu na mtu anaweza kusema elimu hutumiwa na akili kuamua njia sahihi.

Dini inasema kwamba ukijifunza jambo, kabla ya kulifanyia kazi unapaswa kufikiria kuona matokeo ya kulifanyia kazi litakuwaje na kama ni sawa kulifanya au la. Ndiyo maana tunasoma katika Hadithi kwamba usingizi wa mwanachuoni ni bora zaidi ya ibada za Jahili (mjinga).

Hekima katika kufuata dini ni tofauti na hekima katika masomo ya dini. Katika kutekeleza mafundishi dini, hekima ina maana ya kuzingatia matokeo. Pia, moja ya ishara za hekima ni mtazamo wa wastani. Kwa mujibu wa Imam Ali (AS), jahili daima hutenda mambo kwa kufurutu ada.

Kigezo kingine cha hekima ni kusisitiza uzoefu. Mtu anapaswa kutumia uzoefu wa zamani na asirudie vitendo ambavyo vimeshindwa kuleta matokeo yaliyotarajiwa hapo awali. Kuna baadhi ya vigezo 20 katika aya za Qur’ani na Hadith vinavyomsaidia mtu kuwa na mwenendo wa busara.

Makala hii ni sehemu ya hotuba ya Hujjatul Islam wa Muslimin Hamid Ridha Shariatmadari mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Madhehebu za Kiislamu Tehran.

captcha