IQNA

Utamaduni wa Kiislamu

Morocco yaandaa maonyesho ya Qur'ani nchini Tanzania (+Video)

18:48 - August 14, 2022
Habari ID: 3475620
TEHRAN (IQNA) – Watanzania wamepokea kwa furaha maonyesho ya uchapishaji wa Qur’ani Tukufu na Hadithi yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

Maonyesho hayo, ambayo yaliangazia mila za Morocco katika kuchapisha na kutangaza Qur'ani Tukufu, yalifanyika pembizoni mwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Wakfu wa Maulamaa wa Afrika wa  Mfalme Mohammed VI  wa Morocco umeandaa maonyesho na na mashindano hayo ambayo yamefanyika katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani na usomaji wa Tajweed na Tarteel.

Mashindano hayo yalihudhuriwa na washiriki 88 kutoka nchi 34. Taasisi kadhaa za Kitanzania na Morocco, zikiwemo Maktaba ya El Hassania, Maktaba ya Kitaifa, Msikiti wa Quaraouiyine, Wakfu wa Mfalme Mohammed VI  wa Morocco na Maktaba ya Ibn Youssef huko Marrakech, zilichangia katika maonyesho hayo.

Tukio hilo lilikuwa ni fursa ya kuwasilisha historia ya Misahafu ya Morocco ikiwa ni pamoja na sanaa ya kupamba Misahafu katika historia yote ya Uislamu nchini humo.

Tanzania Hosts Quran Manuscripts, Publication Exhibition (+Video)

Wakfu wa Maulamaa wa Afrika wa  Mfalme Mohammed VI  , kwa mujibu wa waanzilishi wake, ni taasisi ya kidini ya Kiislamu inayotaka kuzuia itikadi kali na kupiga vita malumbano ya kimadhehebu ndani ya Uislamu.

Lengo la msingi ni kuunganisha na kuratibu juhudi za wasomi  wa Kiislamu kutoka Morocco na nchi nyingine za Afrika ili kuunganisha maadili ya Kiislamu ya kustahamiliana.

Pia wakfu huo unalenga kuwezesha hatua za kiakili, kisayansi na kitamaduni kwa kuwaleta pamoja na wasomi Waislamu kutoka duniani kote ili kuhimiza uanzishwaji wa vituo vya kidini, kisayansi na kitamaduni na kufanya kazi kuelekea kufufua urithi wa pamoja wa kitamaduni wa Kiafrika, wa Kiislamu.

3480080

captcha