IQNA

Kuamurisha mema na kukataza maovu

Yanayohitajika katika kukataza maovu katika Uislamu

17:31 - August 15, 2022
Habari ID: 3475628
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa Fiqh ya Kiislamu, baadhi ya masharti yanatakiwa kutekelezwa linapokuja suala la kutekeleza agizo la Qur’ani la kuwakataza wengine kufanya maovu.

Kuamurisha mema na kukataza maovu ni miongoni mwa mafundisho muhimu ya Uislamu. “Na siku atakapo wakusanya wao na hao wanao waabudu, na akasema: Je! Ni nyinyi mlio wapoteza waja wangu hawa, au wao wenyewe walipotea njia? (Sura Luqman, aya ya 17)

Hujjatul Islam Mohammad Soroush Mahallati, msomi wa chuo cha Kiislamu Qom, alionyesha baadhi ya masharti yanayohitajika kwa agizo hili. Huu hapa ni muhtasari wa matamshi yake:

Imam Hussein (AS) alisimama kupigana na batili. Huku tukiwa katika mwezi wa Muharram wa kukumbuka mwamko  mkubwa wa Imam Hussein (AS) siku hizi, ni fursa nzuri ya kutazama ndani zaidi na kugundua udhaifu wetu. Imamu Husein (AS) kabla ya kuelekea Karbala alisema: “Siondoki (Madina) kama muasi, mkandamizaji na mchupa mipaka, bali madhumuni yangu ni kuurekebisha Umma wa babu yangu. Njia pekee ya kufanya mageuzi haya ni kwa Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu"

Jamii iliyoathiriwa na matendo mabaya ni kama mji ulioathiriwa na tetemeko la ardhi au mafuriko. Kutumia mwongozo wa Qur'ani ndio njia ya kupigana na maovu katika jamii. Lakini jitihada hii ina masharti fulani.

Masharti ya kuamrisha mema. Marehemu Marja Ayatullah Safi Golpaygani alitoa fatwa juu ya suala hili kwani alikuwa makini kuhusu mema na mabaya katika jamii.

Aliulizwa juu ya mipaka na viwango vya kuamrisha mema na kukataza maovu.

Akiitaja amali hii kuwa miongoni mwa amali muhimu, alibainisha kuwa kuamrisha mema na kukataza maovu kuna mambo mengi na kwamba baadhi ya mambo nyeti yanapaswa kuzingatiwa wakati wa kuyatekeleza.

Fatwa yake inasisitiza kuwa kuamrisha mema na kukataza maovu kunapasa kutekelezwa kwa ufanisi na njia inayokubalika. Alisem kitendo hicho hakipaswi kuwaongoza wengine kuchukia dini, kuutambulisha Uislamu kama dini yenye jeuri, na kumfanya anayefanya kitendo hicho awakasirishe watu

Katika fatwa hii, Ayatullah Safi Golpaygani alibainisha kwamba baadhi ya nukta hizo zinapaswa kuzingatiwa ili kuamrishana mema na kukataza maovu kuweze kuwa na ufanisi na kukubalika.

captcha