IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa

Mashahidi wa Ashura wanalihutubu taifa la Iran na wapiganaji mashujaa wa Syria, Iraq, Palestina na Lebanon

19:44 - August 19, 2022
Habari ID: 3475645
TEHRAN (IQNA)- Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema, kwa muda wote walipokuwa wakishikiliwa mateka, mateka wa kivita wa Iran walizigeuza kambi za Kibaathi madrasa za mafunzo na mafundisho ya Ashura.

Agosti 17, 1990 Iran ya Kiislamu ilishuhudia tukio la kurejea nchini mateka waliokomboka na waheshimika, ambao baada ya miaka kadhaa ya kuishi kizuizini kwenye jela za kutisha na kuogofya za utawala wa Baathi wa Iraq, waliweza kukanyaga tena ardhi ya Iran ya Kiislamu.

Kurudi nchini mateka hao waliokomboka, baada ya miaka kadhaa ya kuhimili na kuvumilia mateso makali kabisa, yalikuwa matunda ya muqawama wa kiwerevu lilioonyesha taifa la Iran katika kukabiliana na adui katika miaka minane ya vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na utawala wa Baathi wa Iraq dhidi ya Iran.

Katika hotuba ya Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, Khatibu wa muda wa Sala hiyo Hujjatul Islam Wal-Muslimin Sayyid Mohammad Hassan Abu Turabi Fard ameashiria tarehe 17 Agosti, inayosadifiana na Mordad 27 kwa kalenda ya Hijria Shamsia, ambayo ni siku walipowasili nchini mateka wa kivita waliokomboka; na akaitaja kumbukumbu hiyo kuwa ni siku kubwa na ya kudhihirika nguvu na uwezo wa nchi. 

Abu Turabi Fard ameongezea kwa kusema: vijana azizi wa Kiislamu, waliacha kumbukumbu ya kuandikwa kwa wino wa dhahabu katika historia ya vita vya Kujihami Kutakatifu katika kipindi cha muongo mmoja wa kushikiliwa mateka; na wakaigeuza Ashura kwa maana yake halisi kuwa nembo na ruwaza ya izza, utukufu na istiqama.

Huku akiashiria kwamba Ashura ndiyo iliyofanikisha Kujihami Kutakatifu, Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema, mashahidi wa Ashura wanalihutubu taifa la Iran na wapiganaji mashujaa wa Syria, Iraq, Palestina na Lebanon ya kwamba, sisi ndio tulioifanya kazi hii; na kazi kubwa na adhimu ya Ashura ndiyo iliyotengeneza fursa hii.

Aidha, Abu Turabi Fard amegusia tukio la Mordad 28, inayosadifiana na Agosti 19, 1953 na akasema, hilo lilikuwa tukio la nakama katika historia ya kisiasa ya Iran, ambapo kwa uongozi wa mashirika ya ujasusi ya Marekani na Uingereza na kwa muda wa robo karne, taifa la Iran lilitaabishwa na utawala wa kidikteta wa Shah uliokuwa kibaraka wa kambi ya Magharibi.

4079175

captcha