IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Hatua ya awali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza Mjini Makka

17:39 - September 11, 2022
Habari ID: 3475767
TEHRAN (IQNA) - Hatua ya awali ya Duru ya 42 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani imeanza nchini Saudi Arabia katika mji wa Makka.

Msikiti Mkuu katika mji mtakatifu wa Mecca ndio mwenyeji wa hafla hiyo, kulingana na tovuti ya Al-Madina.

Ikiandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, duru ya awali ya Tuzo ya Qur'ani ya Mfalme Abdul Aziz ilianza Jumamosi.

Itaendeshwa kwa siku tatu huku washindani wakichuana katika vipindi vya asubuhi na mchana.

Kuhifadhi Quran, usomaji na Tafseer (tafsiri) ni kategoria za mashindano.

Washindi wakuu wa hatua hii watatinga fainali.

Jumla ya wahifadhi na wasomaji Qur'ani 146 kutoka nchi 103 walishiriki katika makala ya 41 ya mashindano hayo yaliyofanyika mwaka 2019.

Mashindano hayo ya Qur'ani yalisitishwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutokana na janga la corona.

4084608

captcha