IQNA

Arbaeen ya Imam Hussein AS

Waislamu Nigeria, Tanzania washiriki maombolezo ya Arabeen ya Imam Hussein AS

21:44 - September 18, 2022
Habari ID: 3475801
TEHRAN (IQNA) -Waislamu ya madhehebu ya Shia Tanzania, visiwani Zanzibar, Nigeria na Niger wameshiriki katika marasimu, matembezi na vikao vya kuadhimisha Arbaeen (Arubaini) ya Imam Hussein (AS).

Huko nchini Nigeria, mamia ya watu walishiriki katika matembezi hayo ya Arubaini ya Imam Hussein (AS) jana Jumamosi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Baadaye walikusanyika katika Husseiniya ya Baqiyatullah katika mji wa Zaria. Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky aliuhutubia mkusanyiko wa waombolezaji hao na kusema, matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS yataendeleaa hadi atakapodhihiri Imam Mahdi AS.

Amesema Waislamu wa Nigeria wamefanya matembezi hayo kwa njia ya amani katika vituo kadhaa katika miji na majimbo ya Kano, Kastina, Zamfara, Sokoto, Kaduna, Bauchi na Plateau.

Jeshi la polisi la Nigeria huko nyuma limekuwa likiwashambulia Waislamu wanaoshiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS na kuua shahidi kadhaa miongoni mwao.

Vikao na matembezi ya tukio la kila mwaka ambalo linaadhimisha siku ya 40 baada ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), Imam wa tatu wa madhehebu ya Shia yamefanyika nchini Niger.

Arbaeen ni neno la Kiarabu ambalo mane yake ni 40.  Katika muktadha huu, ni siku ya 40 tangu maadhimisho ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba wake watiifu tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura. Mtukufu huyo aliuawa shahidi katika mapambano ya Karbala  karne 14 zilizopita.

Siku ya Imam Hussein (AS) ya Arbaeen inakuja tarehe 20 Safar, mwezi wa pili wa kalenda ya Kiislamu ya Hijria Qamaria na mwaka huu imesadifiana na 17 Septemba.

3480531

captcha