IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Wawili wauawa kwa kupigwa risasi karibu na Msikiti Marekani

23:48 - September 21, 2022
Habari ID: 3475820
TEHRAN (IQNA) - Wanaume wawili walipigwa risasi na kuuawa Jumatatu usiku huko nchini Marekani katika jiji la Oakland wakati washambuliaji wengi waliokuwa kwenye gari walipofyatua risasi kwa umati wa watu karibu na Kituo cha Kiislamu cha Oakland.

Wanachama wa kituo hicho walibaini kuwa watu hao walikuwa wakisibuiri kupata chakula baada ya kuswali msikitini.

Idara ya Polisi ya Oakland ilisema awali ilipokea tarifa kuhusu risasi nyingi zilizofyatuliwa kabla ya saa mbili kasorobo usiku. Ufyatuaji risasi huo ulitokea karibu na soko la chakula na Mkahawa wa Layalina. Katika eneo la tukio, maafisa waliwakuta wanaume wawili, wenye umri wa miaka 27 na 59, wakiwa na majeraha ya risasi, idara hiyo ilisema. Mwanamume mwenye umri wa miaka 19 alijiendesha mwenyewe hadi hospitali ya eneo akiwa na majeraha yasiyo ya kutishia maisha, polisi walisema.

Wanachama wa jumuiya ya Oakland Islamic Center wanasema wanaume wawili waliofariki walikuwa miongoni mwa karibu watu 100 waliokuwa wamekuja msikitini kwa ajili ya sala ya jamaa na kisha kujumuika katika kula chakula na waumini wenzao.

Kituo cha Kiislamu cha Oakland kilifunguliwa mwaka wa 1990 na ni mahali pa kukusanyika kwa Waislamu, ambapo kuna madarasa na msikiti.

3480577

captcha