IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qari wa Iran aibuka wa Kwanza katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Croatia

20:01 - September 25, 2022
Habari ID: 3475838
TEHRAN (IQNA) - Mwakilishi wa Iran katika Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Croatia alitwaa tuzo ya juu katika kategoria ya qiraa au kisomo.

Ali Reza Mokari alitangazwa mshindi wa juu katika usomaji wa Qur'ani na jopo la majaji.

Shindano hilo lilianza katika mji mkuu wa nchi ya Uropa wa Zagreb mnamo Alhamisi, Septemba 22 na kumalizika kwa hafla ya kukabidhi tuzo Jumamosi, Septemba 24.

Mwaka jana, Sina Tabbakhi wa Iran pia alikuwa wa kwanza katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu baada ya kushindana na washiriki 33 kutoka nchi 26.

Ali Reza Mokari aliyezaliwa mwaka wa 2005 katikati mwa jiji la Isfahan, ni mwanafunzi wa Shahda ya Uzamili katika fani ya Qur'ani na Hadithi katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Mafundisho ya Qur'ani Iran.

Amewahi kushinda vyeo mbalimbali katika mashindano ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa, ikiwa ni pamoja na tuzo ya juu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat mwaka jana.

Msomaji huyo mchanga wa Qur’ani alikuwa mjumbe wa Msafara wa Qur'ani wa Nuru (Nuru) wa Iran ambao ulifanya programu za Qur'ani katika miji mitakatifu ya Makka na Madina wakati wa Hija mapema mwaka huu.

Katika miaka ya hivi karibuni, wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani wa Iran wamepata mafanikio makubwa katika matukio mbalimbali ya kimataifa ya Qur'ani yaliyofanyika katika nchi kama vile Malaysia, Russia, Kuwait, Uturuki na Croatia.

4087859

captcha