Shirika rasmi la Habari la Imarati WAM, limesema kwamba kikao hicho kimeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiislamu Isesco, kwa ushirikiano wa Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu. Isesco ilitangaza Ijumaa kwamba lengo la kuandaliwa kikao hicho cha siku mbili cha kimataifa ni kuenezwa mipango ya kistratejia katika nyanja za mafunzo ya nguvu kazi ya kutegemewa na kubadilishaana uzoefu wa nchi za Kiislamu katika uwanja huo. Taarifa ya shirika hilo, imesema kuwa, washiriki wasomi watakaohudhuria kikao hicho watabadilishana mawazo na uzoefu wao kuhusiana na jinsi ya kuanzisha kituo cha Kiislamu cha soko la ajira. Mwishoni, taarifa hiyo imesema kuwa wahadhiri kutoka nchi za Asia na Afrika watashiriki katika kikao hicho na kujadili pia suala la kuimarisha uhusiano wa vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu na kuanzisha soko la ajira la nchi za Kiislamu kwa madhumuni ya kutoa mafunzo kwa nguvu kazi ya kutegemewa katika nchi za Kiislamu. 320448