IQNA

Mwandishi mmoja wa gazeti nchini Ufaransa ahukumiwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu

8:07 - November 22, 2008
Habari ID: 1710784
Mahakama ya mji wa Toulouse nchini Ufaransa imemuhukumu kifungo cha miezi mitatu jela Rodolf Grivel, mhariri mkuu wa gazeti la 'Kusini' la mji huo kwa kuchapisha makala inayowakashifu Waislamu na kuamusha hisia za ubaguzi wa rangi dhidi yao.
Hukumu hiyo ilitolea siku chache zilizopita kufuatia malalmiko ya jumuiya ya kupambana na ubaguzi wa rangi na jumuiya kadhaa za Kiislamu za mji wa Toulouse kwa viongozi husika. Kuhusiana na suala hilo, jumuiya za Kiislamu katika mji huo zimesema hiyo ni mara ya kwanza kwa mwandishi gazeti huyo kuchukuliwa hatua kama hiyo ya kisheria kwa sababu huko nyuma, Waislamu wamekuwa wakilalamika sana dhidi yake kuhusiana na makala za ubaguzi anazoandika katika gazeti lililotajwa, lakini bila ya kuchukuliwa hatua yoyote na vyombo husika. 323010
captcha