Gazeti la Morocco la al Maghribiya limeandika kuwa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC waliokutana mjini Cairo kuchunguza mchango na nafasi ya mwanamke katika ustawi wa nchi za Kiislamu, wameitangaza tarehe Mosi Oktoba kuwa Siku ya Mshikamano wa Kiislamu na Wanawake na Watoto na Waathirika wa Vita na Uvamizi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Lengo la hatua hiyo limetajwa kuwa ni kutoa himaya na msaada wa kimaada na kiroho kwa wanawake na watoto katika nchi za Kiislamu na kupinga vita na uvamizi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Mkutano wa pili wa kimataifa wa kuchunguza Nafasi ya Wanawake Katika Ustawi wa Ulimwengu wa Kiislamu ulimalizika jana mjini Cairo. 325685