IQNA

Nakala ya maandishi ya mkono ya Injili ya Yohana kupigwa mnada mjini London

15:04 - December 01, 2008
Habari ID: 1714697
Sehemu ya nakala ya kale ya maandishi ya mkono ya "Injili ya Yohana" inayorejea kwenye karne ya pili Miladia itauzwa katika mnada wa London, Uingereza.
Nakama hiyo ya kale ya Injili ya Yohana imeandikwa kwa lugha ya Kigiriki mwaka 200 baada ya kuzaliwa Yesu na inatazamiwa kwamba itauzwa kwa kiasi cha dola laki nne na sitini elfu.
Mtaalamu wa nakala za maandishi ya kale ya mkono wa London Timothy Bolton anasema: Nakala hiyo ni ya kwanza au ya pili ya kale ya Injili ya Yohana ambayo ndiyo Injili bora na mashuhuri zaidi ya nakala zilizoandikwa kwa mkono za Injili.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa kipande hicho cha nakala ya zamani ya Injili ya Yohana kilipatikana mwaka 1922 katika eneo lililoko umbali wa kilomita mia mbili kutoka Cairo nchini Misri ambako ndiko lilikoishi kundi la kwanza la Wakristo. Watalaamu wa mambo ya kale wanaamini kwamba nakala hiyo ya Injili ya Yohana iliandikwa katika mji wa Alexandria, Misri. 327810



captcha