IQNA

Jumuiya ya Wanafikra na Waandishi wa Iraq yalaani kupasishwa makubaliano ya kiusalama

9:55 - December 02, 2008
Habari ID: 1714886
Jumiya ya Wanafikra na Waandishi wa Iraq imetoa taarifa ikilaani kupasishwa makubaliano ya kiusalama ya Washington na Baghdad na kusema kuwa makubaliano hayo hayana mashiko ya kisheria.
Taarifa hiyo imesema: Waliotia saini makubaliano hayo ndio wanaobeba lawama na jukumu la kihistoria na kimaadili la kuyapasisha.
Jumuiya ya Wanafikra na Waandishi wa Iraq imesisitiza kuwa haitatambua rasmi vipengee vya makubaliano hayo ya kiusalama kati ya Baghdad na Washington na imewataka wanaharakati na wasomi wa nchi hiyo kuunda kambi moja ya kuyapinga. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, makubaliano hayo yatakuwa na taathira mbaya kwa uhuru, kujitawala, mamlaka ya ardhi ya Iraq na maslahi ya taifa.
Jumuiya ya Wanafikra na Waandishi wa Iraq imefananisha makubaliano ya kiusalama ya Baghdad-Washington na mkataba wa serikali ya kikoloni ya Uingereza na Iraq katika nusu ya kwanza ya karne ya 20 na kusisitiza kwamba azma ya wananchi wa Iraq itazuia utekelezwaji wa vipengee vya makubaliano hayo. 328265

captcha