Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Jordan, waandamanaji hao wamemkabidhi mwanadiplomaisa mwandamizi wa ubalozi wa Misri taarifa yao na kumtaka aifikishe kwa wakuu wa serikali ya Cairo.
Waandamanaji mbali na kulaumu jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel, wametoa wito kwa serikali ya Misri kufungua haraka kivuko cha Rafah na kuruhusu bidhaa za dharura kuwafikia raia wanaoteseka wa Ukanda wa Ghaza na vile vile kuwaruhusu wagonjwa mahututi kutoka nje ya ukanda huo ili waweze kupata matibabu kwingineko.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari wa Meno wa Jordan Dkt. Mustafa Ar-Rashdan amehutubiu maandamano hayo akisema, leo Wapalestina wanaishi katika mazingiria magumu na ya hatari na kwamba wanakabiliwa na jinai za kinyama zaidi dhidi ya binaadamu. Dkt. Ar-Rashdan ameongeza kuwa wakaazi wa Ghaza wanaishi katika mzingiro wa kinyama unaotekelezwa na utawala haramu wa Israel. Amesema, Ukanda wa Ghaza unakumbwa na mkasa mkubwa wa kibinaadamu baada ya utawala wa Kizayuni kuzuia chakula, madawa, mafuta na umeme kuingia katika ukanda huo.
Katika taarifa yao waandamanaji hao pia wamemtaka Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kulipa kipaumbele suala la kuvunja mzingiro wa Ghaza. 329905