IQNA

Taarifa ya Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu kuhusu maafa ya Gaza

11:35 - December 13, 2008
Habari ID: 1718432
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imetangaza kuwa, mashambulio ya kijeshi yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza, Palestina inayokaliwa kwa mabavu, ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya Waislamu na maafa ya kibinadamu ni ina fulani ya mauaji ya kizazi.
Taarifa hiyo imesema: Mashambulizi hayo yanakiuka sheria za kimataifa na ni jinai za kivita.
Taarifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imeongeza kuwa maafa hayo yametokana na kimya cha jamii ya kimataifa kuhusiana na matukio ya Palestina. Taarifa ya taasisi hiyo imebainisha kwamba, duru mpya ya mashambulio ya Wazayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kushadidi hali mbaya ya kimaisha ya wananchi hao kunatokana na jamii ya kimataifa kunyamazia kimya jinai za Wazayuni hao maghasibu na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na jinai hizo.
Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imelaani vikali kimya cha jamii ya kimataifa na kuikosoa pia misimamo dhaifu ya nchi za Kiarabu. Imesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaungwa mkono na maadui wote wa Uislamu hususan Marekani ambayo inausaidia kimaada, kijeshi, kisiasa na kidiplomasia ili uendelee kutenda jinai dhidi ya umma wa Kiislamu.
Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu imezitaka jumuiya za kutetea haki za binadamu hususan Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) kufanya juhudi za kuzuia maafa hayo ya Gaza. 332478
captcha