IQNA

Watoto wa Lebanon waandamana kutetea wenzao wa Ukanda wa Gaza

15:37 - December 15, 2008
Habari ID: 1719490
Watoto wadogo wa Lebanon wameandamana mjini Beirut wakionyesha uungaji mkono wao kwa wenzao wanaoteseka katika Ukanda wa Gaza kutokana na mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo hilo.
Waandamanaji hao watoto wamelaani kimya cha jamii ya kimataifa na upuuzaji wa Umoja wa Mataifa kuhusu maafa yanayowapata watoto wa Ukanda wa Gaza.
Watoto hao waliokuwa na mabango yenye maandishi yanayolaani jinai za Israel huko Palestina, wametoa wito wa kurejeshwa haki zilizoghusubiwa za taifa la Palestina.
Waandamanaji hao pia walifunga mikono yao kwa minyororo ikiwa ni ishara ya mashaka yanayowasibu watu wa Gaza wanaozingiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mmoja kati ya watu waliohutubia maandamano hayo ya watoto mjini Beirut amehoji, ni dhambi gani iliyofanywa na watoto wa Gaza ili waadhibiwe kiasi hiki? Je, dhambi yao ni kuwa walizaliwa katika eneo hilo? Ameilaumu pia jamii ya kimataifa kwa kuwaacha watoto wa Ukanda wa Gaza katika mikono ya katili muuaji. 333802



captcha