Isam Sultani amesema: Kitendo cha kupeana mikono Sheikh wa al Azhar na Rais wa utawala haramu wa Israel Shimon Peres wakati wa mkutano wa dini mjini New York, Marekani na matamshi yake kwamba hana habari ya mzingiro wa Gaza unaofanywa na Israel dhidi ya wakazi milioni moja na nusu wa eneo hilo, vinakinzana na mada ya 30 ya katiba ya al Azhar.
Amesisitiza kuwa wanachama wengi wa taasisi hiyo wanaunga mkono suala la kupokonywa uanachama Sheikh Tantawi kwani kukubali kiongozi huyo suala la kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel kunatoa picha isiyokuwa sahihi kwa walimwengu kuhusu taasisi ya kidini ya al Azhar.
Kiongozi wa chama cha al Wasat amesema kuwa, kitendo cha Tantawi cha kupeana mkono na Shimon Peres kimekiuka maamuzi na sheria zote za al Azhar na Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya chuo hicho ambazo zinasisitiza kuwa ni kosa la kisheria kuamiliana na utawala ghasibu wa Israel. 334127