IQNA

Waziri wa haki za binadamu wa Yemen ataka jamii ya kimataifa kusitisha jinai za Wazayuni huko Gaza

18:25 - December 15, 2008
Habari ID: 1719541
Waziri wa Haki za Binadamu wa Yemen Huda Alban ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti kusitisha jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia huko Gaza.
Huda Alban amenukuliwa na shirika la habari la Sabanews akisema kuwa, uvamizi wa Wazayuni huko Gaza unakiuka maazimio yote ya Umoja wa Mataifa na mikataba mbalimbali ya haki za binaadamu hasa mkataba wa Geneva.
Waziri huyo wa Yemen amesema: Nchi za Kiarabu zinabeba majukumu mazito na zinapaswa kuwanusuru Waarabu wa Palestina na Iraq ambao ardhi zao zinakaliwa kwa mabavu na Marekani na Israel. 334094


captcha