Familia ya mwandishi habari wa Iraq aliyempopoa kwa viatu Rais George Bush wa Marekani imesema kuwa, kitu kilichomkasirisha na kumtia hamasa ya kumrushia viatu kiongozi huyo ni kitendo cha askari wa Marekani cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Familia hiyo inasema: Muntadhir Zaydi, mwandishi na ripota wa kanali ya televisheni ya al Baghdadiyya, aliwaona askari wa Marekani wakikivunjia heshima kitabu cha Qur'ani Tukufu kwa kilenga kwa risasi kitabu hicho katika mji wa Ridhwaniya ulioko magharibi mwa Iraq.
Udai, ndugu wa kiume wa Muntadhir Zaydi ambaye amekuwa shujaa katika ulimwengu wa Kiarabu baada ya kumrushia viatu Rais George Bush wa Marekani, anasema kuwa suala hilo lilikuwa likimkera mno kaka yake na kwamba, aliathiriwa mno na taswira za vita na ukatili wa askari wa Marekani nchini Iraq. Udai amesema: mambo hayo yote yalikuwa chachu iliyomfanya amshambulie Bush kwa viatu.
Muntadhir Zaydi ambaye huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, anashikiliwa na vyombo vya usalama vya Iraq katika eneo lenye ulinzi mkali na familia yake hairuhusiwi kukutana naye. 336260