Rais Ali Abdallah Swaleh wa Yemen amelaani vikali hujuma ya kinyama iliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa uzembe wa Baraza la Usalamala Umoja wa Mataifa kuhusiana na jinai za utawala huo dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi, ndio uliopelekea utawala huo kutekeleza mauaji ya umati dhidi ya raia hao wasio na hatia na hivyo kusababisha Jumamosi nyeusi na ya umwagaji damu dhidi yao.
Akizungumza hivi karibuni mbele ya waandishi habari, Ali Abdallah Swaleh amesema kuwa, kuzembea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kuondoa mzingiro unaotekelezwa na utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kutotoa mashinikizo yoyote dhidi ya utawala huo, ni jambo ambalo limeupelekea utawala huo kumea pembe na kuzidisha hujuma na jinai zake dhidi ya Wapalestina, jambo ambalo limethibitika wazi katika mashambulio yake ya kinyama ya siku ya Jumamosi dhidi ya watoto, wanawake, wazee na vijana wakazi wa Ukanda wa Gaza. Amesema, mashambulio hayo ni ishara ya wazi ya unyama wa utawala huo wa kibaguzi na kulitaka Baraza la Usalama lichukue hatua za dharura kwa lengo la kukomesha mashambulio hayo ya Wazayuni dhidi ya watu wasio na hatia. Wakati huohuo, Rais Abdallah Swaleh ametaka kufanyika kikao cha dharura cha nchi wanachama wa Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC kwa ajili ya kusimAmisha mara moja mashambulio ya kijeshi ya utawala wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza. Siku ya Jumamosi, ofisi ya Rais Abdallah Swaleh pia ilitoa taarifa ikilaani kitendo cha utawala wa Israel cha kuwashambulia kinyama Wapalestina wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. 339448