Katika hali ambayo idadi ya mashahidi wa Palestina waliouwa katika mashambulio ya kinyama ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza imefika zaidi ya watu 1200, nusu yao wakiwa ni watoto na wanawake wasio na hatia, Mordokhai Elyahoo, kuhani mkuu wa zamani wa Mayahudi ametoa ujumbe wa kibaguzi akiwamtaka Ehud Olmert, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel adumishe mauaji ya umati dhidi ya wakazi wa Gaza.
Elyahoo amemtaka Olmert katika ujumbe wake huo aendelee kuwaua kwa umati na bila kusita watu wa Gaza hata wakiwemo wanawake na watoto.
Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la al-Watan, Elyahoo ameandika katika ujumbe huo ambao pia amewatumia watawala wengine wote wa Kizayuni, akisema kuwa kwa mujibu wa maandiko ya Torati Mayahudi wanaruhusiwa kuwaua kwa umati maadui wao na kwamba jambo hilo ni miongoni mwa maadili ya vita ya Mayahudi. Kuhani huyo anaendelea kumshawishi Olmert katika ujumbe huo aendelee kutekeleza mauaji ya umati dhidi ya wakazi wa Gaza akisema kuwa mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina wasio na hatia ni jambo linaloruhusiwa na sheria za Kiyahudi.
Kuhani huyo pia ameazimia kuchapisha ujumbe huo kwa sura ya kijitabu kidogo na kisha kukisambaza katika hekalu zote za Mayahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ili kupata uungaji mkono wa fikra za Mayahudi na Wazayuni waliowengi katika ardhi hizo.
Ni vyema kukumbusha hapa kwamba baadhi ya mauaji ya umati ambayo yamekuwa yakitekelezwa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi yamekuwa yakichochewa na fatuwa kama hizo ambazo zimekuwa zikitolewa na makuhani wenye fikra potofu miongoni mwa Mayahudi. Mauaji ya kinyama ambayo yamekuwa yakitekelezwa na watawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza kwa hakika yamekuwa yakichochewa na fikra kama hizo potofu.
Baadhi ya makuhani kama hao wenye fikra za kibaguzi hata wamekuwa wakisema kuwa serikali ya utawala haramu wa Israel inapasa kujenga kitongoji na shule moja ya kidini ya Mayahudi iwapo Myahudi mmoja atauliwa na Mpalestina. 349390