IQNA

Imamu wa swala ya Ijumaa ya Nafaf:

Fatuwa za mawahabi za kuharamisha maandamano dhidi ya Wazayuni zinasikitisha.

12:14 - January 18, 2009
Habari ID: 1732413
Imamu wa swala ya Ijumaa ya mji mtukufu wa Nafaj nchini Iraq Sayyid Sadruddin Qubanchi amekosoa vikali hatua ya baadhi ya maulamaa wa kiwahabi wa Saudi Arabia ya kutoa fatuwa ya kuharamisha maandamano dhidi ya Wazayuni wa Israel na kuwakufurisha maandamanaji.
Hujjatul Islam Walmuslimin Qubanchi amesema kuwa, fatuwa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Majaji wa Saudi Arabia Sheikh Saleh al Lahidan na baadhi ya maulamaa wa kiwahabi wenye misimamo mikali nchini humo ambayo inaharamisha maandamano ya kupinga jinai za Wazayuni huko Gaza na kuwakufurisha waandamanaji, inastaajabisha na kusikitisha mno.
Amesema: Mawahabi ni kundi lililopotea ambalo linajiona kuwa ndilo Uislamu na kwamba Waislamu waliamka Masuni kwa Mashi hawajali wala kutilia maanani mitazamo ya kundi hilo lenye chuki za kimadhehebu.
Sayyid Sadruddin Qubanchi amesema kuwa, mgogoro wa Gaza si suala la kisiasa pekee bali wakazi wa eneo hilo ni sehemu ya umma wa Kiislamu ambao ni wajibu kwa Waislamu kutetea haki zao. Kwa msingi huo Waislamu wanapaswa kufanya maandamano dhidi ya Israel na kuonyesha mshikamano wao na watu hao wasiokuwa na hatia.
Imamu wa swala ya Ijumaa ya mji mtukufu wa Najaf amekosoa pia misimamo dhaifu ya baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu kuhusu kadhia ya Gaza na akasema: Katika kipindi cha zaidi ya wiki tatu zilizopita utawala wa Kizayuni wa Israel umeshambulia kwa mabomu shule, na makazi ya raia na kuwaua wanawake na watoto wadogo wasiokuwa na hatia yoyote. 349451
captcha