Abu Bakr al-Muflihi, Waziri wa Utamaduni na kundi la wasanii wa Yemen wamehudhuria ufunguzi wa maonyesho hayo ambayo lengo lake kuu ni kuonyesha mfungamano na watu wa Gaza pamoja na kuwashurukuru viongozi wa mapambano ya Wapalestina kutokana na ushupavu wao katika kukabiliana na jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia.
Zaidi ya vikaragosi 70 vinaonyeshwa katika maonyesho hayo. Vikaragosi hivyo vinajaribu kuonyesha jinsi watawala wa Kiarabu walivyozembea na kuonyesha udhaifu mkubwa katika kusimamisha jinai za Wazayuni huko Gaza na mauaji ya kinyama ya Wazayuni hao dhidi ya watoto na wanawake wasio na hatia.
Sehemu nyingine ya maonyesho hayo pia ina vikaragosi vinavyohusiana na suala la Muntadhir az-Zeydi, mwandishi wa Kiiraqi, aliyerusha na kumpopoa kwa viatu Rais Bush wa Marekani na kusema kuwa, hatua hiyo ni zawadi kwa Bush kutokana na uungaji mkono wake kwa mashambulio ya kinyama ya utawala wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia.
Ad'nan al-Mahaqiri, msanii wa Yemen amesema kuwa lengo la maonyesho hayo ya vikaragosi ni kuonyesha mfungamano na wakazi wa Ukanda wa Gaza na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wakazi hao. Ameongeza kuwa maonyesho hayo yana lengo la kuonyesha hasira ya Waislamu dhidi ya kimya cha Waarabu na taasisi za kimataifa mbele ya jinai na mauaji ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. 351461