Maafisa wa jeshi la Israel ni miongoni mwa watu waliozuiwa kufanya safari katika nchi kadhaa ikiwemo Ubelgiji kutokana na jinai zilizofanyika huko Gaza.
Habari zinasema kuwa mashtaka yaliyowasilishwa mahakamani mwaka 2002 dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon kwa kutenda mauaji dhidi ya Wapalestina yamepata nguvu zaidi kwa kuunganishwa na kesi ya sasa na mashambulizi ya utawala huo wa kigaidi katika Ukanda wa Gaza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel Tzipi Livni pia amevunja safari yake nchini Ubelgiji baada ya ukurasa mmoja wa intaneti kuandika kuwa, kiongozi huyo anasakwa kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza. 355810