IQNA

Sherehe ya kuenziwa mbunge wa kwanza wa Kiislamu katika bunge la Scotland

10:21 - February 09, 2009
Habari ID: 1741980
Sherere ya kuenziwa Bashir Ahmad, mbunge wa kwanza Muislamu katika Bunge la Scotland, imeandaliwa na kufanywa na Waislamu wa nchi hiyo.
Shirika la habari la Ufaransa AFP limeandika kwamba Alex Salmond, Waziri Mkuu ambaye pia ni mkuu wa Chama cha Taifa cha Scotland amehudhuria sherehe hiyo na kumshukuru shakhsia huyo wa Kiislamu na kusema kuwa alikuwa mtu mwenye itibari kwa nchi na dini yake. Ameendelea kusema kuwa, alikuwa Muislamu wa kwanza wa chama hicho na mzalendo halisi.
Bashir Ahmad ambaye alichaguliwa rasmi mwaka 2007 kuwa mwanachama wa kwanza Muislamu wa Chama cha Taifa, aliaga dunia huko Glasgow siku ya Ijumaa tarehe 6 Februari. Bashir Ahmad ambaye alizaliwa nchini India na kisha kuhajiri na kwenda Pakistan akiwa na umri wa miaka 21, alihamia Scotland na kisha kufanya juhudi kubwa za kujiunga na Chama cha Taifa ambapo alifanikiwa kufikia lengo lake mwaka 2007. Baada ya ushindi huo, alikuwa akihudhuria vikao vya Bunge huku akiwa amevalia vazi la taifa la Pakistan.
Bashir Ahmad aliapishwa kwa lugha ya Kiurdu na kutangaza kwamba, kujenga shule za watoto wa Kiislamu nchini Scotland ilikuwa miongoni mwa mipango yake muhimu. 361247
captcha