Dakta Ali Larijani amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaitambua Bahrain kuwa ni nchi rafiki na jirani mwema.
Ameashiria kadhia ya Palestina na akasisitiza juu ya udharura wa kuzidishwa mashauriano na juhudi za kidiplomasia kati ya nchi za Kiislamu kwa ajili ya kutatua matataizo ya Wapalestina katika eneo la Ukanda wa Gaza. Amesema kuwa hii leo kuna udharura wa kufanyika juhudi za kuwanusuru watu wa Gaza kutokana na mashaka makubwa yanayowakabili.
Spika wa Bunge la Iran amemwalika mwenzake wa Bahrain kushiriki katika mkutano wa Mabunge utakaofanyika mjini Tehran kujadili hali ya Palestina.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Bahrain Ali bin Saleh amesisitiza juu ya udharura wa kushirikiana katika kudhamini maslahi ya pande hizo mbili. Amesema kuwa ujumbe wa ngazi za juu wa Bunge la nchi hiyo utashiriki katika mkutano ujao wa Palestina njini Tehran. 368212