Huku ikiashiria njama za utawala huo za kuwafukuza Wapalestina kutoka katika ardhi na makazi yao katika mji huo, kamati hiyo imesema kuwa utawala huo una lengo la kuwafukuza Wapalestina wapatao 1500 kutoka katika eneo la Bustan karibu na Msikiti wa al-Aqsa na kuharibu nyuma zao zipatazo 88.
taarifa hiyo Imesisitiza kwamba, njama hizo zina lengo la kuharibu kabisa muundo wa mji huo mtukufu na kuufanya kuwa na utambulisho wa Kiyahudi. Taarifa ya kamati hiyo imeendelea kusema kuwa, wakazi wa Kipalestina wa mji huo ambao wametengwa na wenzao na ukuta wa kibaguzi uliojengwa hivi karibuni na Wazayuni katika eneo hilo, kwa hakika wamezingirwa na kulazimishwa kuishi kama wafungwa.
Imesema, Wapalestina hao wamenyimwa kabisa uwezekano wa kuwa na mawasiliano na ulimwengu wa nje. Hata hivyo, taarifa hiyo inasisitiza kwamba jambo hilo halipasi kuwafanya Wapalestina kuendelea kunyimwa haki zao za kimsingi, ikiwemo ya kurejea katika ardhi zao za jadi. 369793