IQNA

Utawala wa Kizayuni wa Israel ni mtenda jinai za kivita

12:52 - March 05, 2009
Habari ID: 1752029
Washiriki wa kikao cha kimataifa cha 'Jinai za Kibinadamu Gaza na Ukiukaji wa Sheria za Kimataifa' wametoa taarifa wakiutaja utawala wa Israel kuwa mtenda jinai za kivita.
Washiriki wa kikao hicho kilichofanyika siku ya Jumatano wamesisitiza kwamba dalili zilizopo zinathibitisha kwamba askari wa utawala wa Kizayuni walihusika moja kwa moja na jinai dhidi ya binadamu pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu.
Wamesema licha ya kuwa askari wa utawala haramu wa Israel wameondoka katika Ukanda wa Gaza lakini hadi sasa wamekuwa wakiingia na kufanya mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya wakazi wa ukanda huo. Wamesisitiza kuwa hatua ya utawala wa Israel ya kushambulia kwa mabomu nyumba, mashule, misikiti na majengo ya umma ni jinai nyingine ya kivita inayopasa kuwafanywa watawala wa Israel wafikishwe katika mahakama ya kimataifa ya jinai.
Washiriki wa kikao hicho wamesisitiza kwamba jinai nyingine ya kutisha iliyofanywa na jeshi la utawala huo dhidi ya watu wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza ni utumiaji wa silaha zilizopigwa marufuku kimataifa dhidi ya wanawake na watoto wasio na ulinzi. Wametaka watawala na makamanda wa kijeshi wa utawala huo wafikishwe mara moja katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa kuhusika na jinai hizo za kivita dhidi ya raia.
Wakati huohuo, wamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mahakama iya ICC kutekeleza majukumu yao ya kisheria na kutekeleza uadilifu dhidi ya wahusika wa jinai hizo. Katika upande wa pili, wamesisitiza haki ya taifa la Palestina ya kuendeleza mapambano ya kutetea haki zake za kimsingi dhidi ya utawala wa Israel.
Serikali mbalimbali za dunia pia zimetakiwa kushirikiana na vyombo husika vya kimataifa kwa ajili ya kufuatilia na kuwatia mbaroni watawala na makamanda wa Israel waliohusika na jinai hizo dhidi ya binadamu. 372764
captcha